0


Bondia Manny Pacquiao amekubali kupambana na Floyd Mayweather kwenye pambano la masumbwi lililopangwa kufanyika May 2.

Mpaka sasa hakuna jibu rasmi kuhusu Mayweather kukubali pambano hili na kama atatia wino kwenye mkataba ambao imeripotiwa atalipwa dola milioni 120 kwa pambano hilo.

Promota wa pambano hili Bob Arum amesema Manny ameshakubali na kwamba pambano litaweka rekodi kwa kuwa pambano lenye tiketi za bei ghali zaidi kwenye histori ya masumbwi duniani.

Pambano litafanyika kwenye ukumbi wa MGM las Vega, siti kwenye ukumbi huo ni 15000, pesa kutoka kwenye watu wanaohudhuria ukijaa ni milioni 40, mapato ya PAY-PER-VIEW ni dola milioni 200.

Post a Comment

 
Top