Muigizaji wa filamu Flora Mvungi ambaye ni mke wa H.Baba, amedai kuna watu waliofika nyumbani kwake zaidi ya mara tatu wakimtaka mfanyakazi wake awape mwanae wa kike, Tanzanite.
Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Flora amesema yupo katika wakati mgumu akihofia mtoto wake kutekwa na watu wasiojulikana.
“Nimepatwa na hofu sijui kama watu wanataka kuiba mtoto wangu ama vipi? Mara ya kwanza walikuja watu wawili, mwanamke na mwanaume wakamwambia dada wa kazi kuwa nimewaagiza wamchukue Tanzanite wampeleke shule, dada akawakatalia,” alisema Flora.
Amedai kuwa baada ya kukataliwa na mfanyakazi wake alikuja mtu mwingine mwanamke wa kiarabu akijifanya ni rafiki yake akiomba kitana achane nywele zake na kwamba aliingia hadi sebuleni akidai aachiwe mtoto lakini msichana wa kazi alikataa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment