Nick wa Pili aka Nick Mweusi, amewataka wasanii kuacha kuanika mahusiano yao ya mapenzi hadharani kwakuwa ni hatari kubwa katika muziki wao.
Nick amesema kuwa kuweka mahusiano ya mapenzi wazi huenda kukaja kuwaharibia kazi zao pamoja na kuwanyima raha.
“Kuanika mahusiano yako ni kujiwekea hatari chochote kitakachokuja kutokea kitakurudia wewe kutoka kwenye public,” alisema rapper huyo.
“Unajua kitu wanachojua watu wawili wakijua watu mia kuna utofauti sana. Msanii anapokuwa ameweka mahusiano yake ujue ni risk kubwa sana, yaani ame risk sana, chochote kitakachotokea baadaye kwa bahati mbaya au mpenzi wake kaonekana kwenye picha tofauti na mtu mwingine au kafanya kitu ambacho sio kizuri na ni kibaya vyote vitakuja kwako. Kwahiyo ni risk kubwa sana inaweza ikakunyima raha sometimes.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment