Home
»
STORY
» Jokate asema wasanii wa nje ni muhimu katika kukuza muziki wa Tanzania
Mwanamitindo, mtangazaji wa TV na msanii wa muziki, Jokate Mwegelo amesema kuwa tabia za wasanii wa ndani kuwashirikisha wasanii maarufu kutoka nje kumeinua na kuendeleza vipaji vya wanamuziki wa Tanzania.
Jokate ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa hali hiyo ndio iliyomsukuma kuanza kuwashirikisha wasanii wa nje katika muziki anaofanya ili akuze kipaji na kutanua soko la muziki wake.
“Jina langu limepiga hatua kubwa katika masuala ya mitindo na ubunifu, hivyo nataka nijulikane zaidi na kwenye muziki, ndiyo maana kwa sasa nguvu zangu nazielekeza huku, tofauti na kwenye mitindo,” alisema Jokate.
Hivi karibuni Jokate aliachia wimbo aliomshirikisha rapper wa Nigeria, Ice Prince uitwao Leo.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.