0
Changamoto kubwa inayomkabili msanii mpya aliyetoa wimbo uliohit, ni kutoa single ya pili inayoweza kufikia ukubwa wa ile ya kwanza. Mo Music ni mfano wa hili.
 Mo Music aliyehit na wimbo wake ‘Basi Nenda, amesema sio kweli kwamba nyimbo zake mbili zilizofuata ‘Almas’ na ‘Simama’ zilibuma kama baadhi ya watu wanavyosema.

“Nilitarajia zifike hapo zilipofika, kwahiyo ni ngazi ambayo mimi nimetengeneza hii ifike hapa na hii ifike pale and then kama sio kesho au Jumatatu naachia ngoma ambayo nategemea itafika kule ninakohitaji ifike,” amesema.

“Kwahiyo kila kazi ninayoitoa nina lengo nataka ifike wapi. Ndio maana nikasema Almas na Simama zimefika sehemu ambayo nilikuwa nahitaji zifike, tofauti na watu wanavyofikiria. Na nilivyotoa Basi Nenda nilitegemea ifike hapo ilipofika.”

Post a Comment

 
Top