“Damian ni mtu ambaye anaombwa collabo na wasanii wakubwa ambao hata mimi nilitamani kuwaomba collabo. Mtu kama Erick Wainaina anataka kufanya kazi na Damian, Rabbit ambaye artist wake alishinda pia anataka kufanya na Damian, pamoja na Jose Chameleone leo nimeongea nae akiwa Canada akisharudi tumalize hiyo kazi ya Damian. We Imagine watu wangapi East Africa wanatamani kufanya kazi na Chameleone, halafu Chameleone ananiuliza oyaa sasa ile kazi ya Damian tunafanya lini.” Alisema AY kupitia E-Newz ya EATV.
“Kazi kubwa ya Damian utaiona, baada ya Maisha Superstar , Damian ndo mtu ambaye walipomaliza mashindano hata kama hakushinda, lakini ndo mtu aliyepewa show kwanza, yaani baada ya mashindano kuisha yeye akaperform Nairobi. Ukiwauliza hata yule aliyeshinda sidhani hata kama ameshapata hata show moja I’Don’t know, nampa pole kwa yeye lakini mwisho wa siku ilikuwa hivyo” alimaliza AY.
Post a Comment