0
Mastaa wengi wameahidi kuhudhuria show ya maalum iliyoandaliwa na rapper Mabeste Jumapili kwenye ukumbi wa New Maisha Club kwaajili ya kuchangisha fedha za matibabu ya mke wake Lisa ambaye pia meneja wake.
Lisa anasumbuliwa na maradhi mbalimbali likiwemo tatizo kwenye ubongo wake. Hivi karibuni Mabeste amekuwa akiendesha kampeni ya kuchangisha fedha kulipia gharama za matibabu yake.

Mastaa walioahidi kuwepo kwenye show hiyo ni pamoja na Vanessa Mdee, Adam Juma, Millard Ayo, Nchakalih, Roma, Diva, Young Killer, Jokate, Hemedy, Kajala, Rose Ndauka, Country Boy na Riyama.

Wengine ni Manecky, Mirror, Pam-D, Quick Rocka, Kajala, Tundaman na wengine.

Kiingilio kwenye show hiyo ni shilingi 10,000 tu.

Post a Comment

 
Top