0
Maswali mengi ambayo wasanii ambao hawajatoa nyimbo kwa muda mrefu hukutana nayo kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa mashabiki wao, huwa ni ‘mbona umekaa kimya’ kutokana na jinsi ushindani ulivyo mkubwa na kila msanii akijitahidi kutoa nyimbo ili watu wasimsahau.
Lakini kwa rapper msomi Hamis “Mwana FA” Mwinjuma yeye anaamini kuwa msanii kukaa kimya inamuongezea heshima kwa mashabiki .

“Unajua mashabiki wamekuwa na fikra potofu, wanapoona msanii yupo kimya akili zao zinawatuma kwamba kaishiwa wakati sivyo,” Mwana FA aliliambia gaeti la MTANZANIA.

Aliongeza kwamba, kukurupuka mara nyingi kumekuwa kukimaliza vipaji vya wasanii kwa haraka na kujikuta hawadumu kwenye fani zao.

Mwana FA ameahidi kuachia wimbo mpya uitwao ‘Sitoi hela’ ndani ya wiki mbili, na itakuwa single inayofuata baada ya ‘Kiboko Yangu’ aliyomshirikisha Alikiba.

Post a Comment

 
Top