0
Young Killer afunguka sababu ya kutonunua gari hadi leo,ajenga nyumba. Staa wa Bongo Fleva,Young Killer amefunguka sababu ya kutonunua gari hadi leo ni kuwa anatumia magari ya marafiki zake kwenye shughuli zake za kawaida na za kisanii na kwamba pesa yake amewekeza kwenye mjengo wake anaoujenga nyumbani kwao jijini Mwanza. Akizungumza na Clouds FM,alisema kuwa ana uwezo wa kupata gari muda wowote akitaka kutoka kwenda sehemu yoyote ndiyo maana hana haraka ya kununua gari. 'Asilimia kubwa ya washikaji zangu wana magari ndiyo maana sina haraka ya kununua gari pesa yangu nyingi nimewekeza kwenye nyumba yangu ninayoijenga nyumbani kwetu Mwanza na mama yangu ndiye anayesimamia ujenzi,'alisema Young Killer


Post a Comment

 
Top