0
Q-Chief ameachia video ya wimbo wake mpya ‘For You’ iliyofanyika nchini Afrika Kusini lakini hiyo haimaanishi kuwa ametosheka. Muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Abubakar Katwila amesema ana mpango pia wa kuwashirikisha wasanii wa kimataifa.

Akiongea na 255 ya XXL kupitia Clouds FM, Chilla amesema menejimenti yake inafanya mazungumzo na wasanii wa Afrika Kusini akiwemo Oskido ili kuangalia uwezekano wa collabo.

Pia amesema amepanga kufanya wimbo mwingine na Christian Bella kwakuwa anaamini kuwa ni muimbaji mwenye kipaji kikubwa.

Post a Comment

 
Top