0
Performance yenye utata iliyofanywa na muimbaji Jennifer Lopez kwenye tamasha kubwa la muziki nchini Morocco, imesababisha wanasiasa wa kiislamu nchini humo kumtaka waziri wa mawasiliano ajiuzulu.
Jennifer Lopez (45) alitumbuiza kwenye tamasha la Mawazine lililofanyika May 29 katika mji mkuu wa Morocco, Rabat ambalo lilioneshwa moja kwa moja na runinga ya 2M ya nchini humo.



Waziri wa mawasiliano wa Morocco, Mustapha Khalfi amekosolewa kwa kuruhusu show ya J.Lo iliyotajwa kuwa ilikuwa ya kuukosea adabu umma kuoneshwa moja kwa moja kwenye runinga.



Watu walikosoa mavazi ya J.Lo na dancers wake pamoja na mapozi ya kucheza ambayo wanadai hayakustahili kuoneshwa moja kwa moja kwenye runinga.

Hata hivyo waziri huyo amekataa kujiuzulu.

Source: BBC

Post a Comment

 
Top