0

Suti ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh Steven Wassira imegeuka gumzo mtandaoni baada ya kukosewa kufungwa vifungo vyake..... Wassira alionekana ndani ya vazi hilo wakati wa Sherehe za Utume zilizoandaliwa na kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) na kujumuisha nchi zingine 11 za Afrika Mashariki na Kati.
Sherehe hizo zilizofanyika juzi uwanja wa taifa Dar zilihudhuriwa na kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson ambapo mgeni rasmi wa sherehe hizo alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh Steven Wassira (wa pili toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson( wa nne toka kushoto) wakati wa sherehe za utume wa kanisa hilo.

Post a Comment

 
Top