Ndugu wa Bobbi Kristina Brown wamekubali kumtolea mashine ya kumsaidia kuishi kesho Jumatano ili afariki katika siku moja aliyofariki mama yake Whitney Houston, vyanzo vimeliambia gazeti la New York Post.
Bibi yake Bobbi, Cissy Houston ndiye aliyetoa wazo hilo la kumtolea mashine hiyo Feb 11 kufuatia mjadala na familia ya Bobby Brown kwenye hospitali ya Emory University jijini Atlanta.
Whitney alifariki Feb 11 mwaka 2012 akiwa bafuni kwenye hoteli ya Beverly Hilton. Bobbi Kristina, 21, ambaye ni mtoto pekee wa Houston na Bobby Brown amekuwa kwenye coma tangu akutwe akiwa hajitambui bafuni Jan 31.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment