Rapper Nay wa Mitego amesema kuwa ametenga bajeti ya shilingi milioni 60 kukamilisha kolabo na msanii wa Nigeria.
Nay amesema kuwa gharama hiyo inajumuisha gharama ya video ambayo amedai atafanya na Godfather wa Afrika Kusini.
“Kolabo sio rahisi kama watu wanavyodhani,” amesema Nay. “Inatakiwa uwe na pesa za kutosha na ujiandae vizuri ndo maana mimi bado najipanga vizuri. Ila tayari maandalizi nimeshaanza, nimejua natakiwa kuwa na nini kwa sasa. Ukiangalia ili uweze kufanya video kali na Godfather sio chini ya milioni ishirini ingawa bado sijajua kama atafanya yeye au nitamsafirisha director wangu Kelvin Bosco kwa sababu hata yeye anaweza kufanya kitu kizuri pia, yote yanawezekana ndo maana nikasema najiandaa.”
“Pia natakiwa kumsafirisha msanii kutoka Nigeria mpaka South, anahitaji treatment ya tiketi ya ndege nzuri anahitaji hoteli nzuri, kwahiyo ni gharama kubwa sana. Ni kama milioni 50 au 60 nadhani inaweza kutosha. Ukiangalia pia na mimi inanibidi nisafiri na team yangu. Kama sio watu wawili au watatu, kwahiyo ni gharama kubwa sana ukiangalia kwa muziki wetu hapa nchini.”
Home
»
Entertainment
»
STORY
» Nay wa Mitego atenga milioni 60 kukamilisha kolabo na msanii wa Nigeria
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment