0
Muimbaji Mandojo amesema sababu za kuwa kimya ni kutokana na muziki wa sasa kuwa na changamoto nyingi tofauti na zamani licha ya kuwa unalipa vizuri kuliko wa zamani.
Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Mandojo alisema mpaka sasa yeye na swahiba wake Domo Kaya wana kazi nyingi zilizo tayari ila hawawezi kuzitoa mpaka wajipange kifedha.

“Sasa hivi watu wananufaika, soko ni zuri, sasa hivi hatuwezi kutoa nyimbo kama zamani ukaitoa tu ili iende yenyewe hufiki popote,” amesema muimbaji huyo.

“Lazima uiwekee mipango, budget ya kutoa nyimbo, bana hii ngoma ilie, lazima ufanye video nzuri inayoeleweka. Kwahiyo muziki umebadilika sana. Muziki umekua sana kuanzia kisoko mpaka kiutayarishaji inabidi. Inabidi ujipange vizuri, tofauti na mwanzo mambo yalikuwa rahisi rahisi Kwetu sisi ni changamoto sana na ukiangalia watu wanazaliwa wapya kwahiyo sasa hivi sisi wasanii wa zamani tuna changamoto.”

Post a Comment

 
Top