“Never! That is my private. Nyumba yangu, boyfriend wangu, mahali naweka kichwa nalala, utaona tu hotel niko vacation and all that, lakini mahali naweka kichwa changu nalala, na mtu aliyeuteka moyo wangu ni vitu ambavyo kamwe siwezi kuweka Instagram, hata familia yangu siwezi kuwaweka Instagram.” Alisema Huddah kupitia Amplifaya ya Clouds Fm.
Ameongeza kuwa picha nyingi ambazo huwa anaweka huwa ni za hotelini pamoja na zake mwenyewe, na haweki picha za mpenzi wake kuhofia wasichana wa mjini wasije kumrubuni na kumpora.
“Huwa naweka zangu tu, watu wanaona mimi mbinafsi kwasababu huwa siweka picha za watu wengine, kwasababu Instagram ina watu wengine wana matusi sana, wakati mwingine unaweza kuweka picha na rafiki yako wanamtusi rafiki yako, sasa imagine uweke mtu kama boyfriend wako halafu tena wasichana wana competition, wakiona ooh huyu ndio boyfriend wa Huddah, wanataka kumfatilia yule jamaa wanam Dm Dm huko ndani picha uchi zingine halafu bado wanakuja kunitusi, I don’t put my private life out there”.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.