0
Lil Wayne na Wiz Khalifa wanaingia kwenye biashara mpya, Udj na wanatoza mkwanja mrefu.
TMZ imeandika kuwa Wayne na Khalifa wamevutiwa na uvamizi wa Snoop kwenye fani hiyo na tayari wameshatangaza bei yao.

Wayne atacheza nyimbo uzipendazo kwa $60,000 na Wiz Khalifa atakuwa akichaji $25,000. Pia watataka kulipwa tiketi ya ndege, daraja la kwanza na huduma ya VIP.

Tayari wote ‘wako booked’ lakini bado wanatafuta show zingine. Wiz tayari ana jina jipya, muite DJ Daddy Cat.

Post a Comment

 
Top