0
Muimbaji Shilole ameitumia safari yake ya Ubelgiji kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja. Baada ya kumaliza show yake ya Ubelgiji, Shishi amepata nafasi ya kushoot video ya wimbo wake ‘Malele’.
Shishi akiwa location-Amsterdam

Shishi ametumia location za nchi tatu ambazo ni Amsterdam-Netherlands, Brussels-Belgium pamoja na Holland. Amesema kuwa kabla hajaondoka Tanzania tayari alikuwa amepanga kushoot video huko.



“Wakati nakuja huku nilikua nimepanga kabisa kwamba nitakuja kushoot na video kutokana mara ya kwanza nilipokuja nilipenda madhari ya huku ya location na vitu vingi tu. So nikasema kwamba nikija kupata kazi tena next time nitakuja kufanya video kwahiyo nikapata tena show, nilipomaliza show nikauliza madirector wa huku nikaambiwa wapo, kuna director anaitwa Lucas anaishi Amsterdam, tukaenda kushoot video huko, tumetumia location za nchi tatu tofauti, tumeshoot Holland, Amsterdam na Brussels. Kwahiyo video kama hivyo ikija kutoka ndio mtaweza kuona nchi ziko tatu tofauti.” Alisema Shishi.



Kuhusu utofauti utakaokuwepo kwenye video hiyo na video zake zilizopita:

“Unajua video zangu nyingi zimekua lazima viuno vionekane kinadada wakicheza sana sana sana sana, mimi nimebadilika kwenye hiyo video, nimeshoot video kiustaarabu zaidi yani kutokana na jinsi location zenyewe zilivyo za kikubwa, kwahiyo ikitoka video unaweza kuona vitu vingi ambavyo nimevifanya, nimeamua kubadilisha pia na rangi ya watu,”.alimaliza Shilole.













Post a Comment

 
Top